Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 20.04.2020: Kane, Bale, Neymar, Lacazette, Dembele, Havertz

Harry Kane
Maelezo ya picha, Je, Juventus kuwapiku Manchester United usajili wa Harry Kane?
Iliyochapishwa

Juventus sasa wanaelekeza nguvu zao kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Tottenham Harry Kane. (Corriere dello Sport - in Italian)

Real Madrid wametoka kwenye kinyang'anyiro cha kumnyakua Harry Kane kutokana na athari za kiuchumi zinazosababishwa na virusi vya corona. (Mail)

Real pia wanafikiria kuwauza wachezaji mpaka sita wa kikosi cha kwanza, akiwemo winga wa Wales Gareth Bale, 30 na kiungo James Rodriguez, 28. (AS)

Neymar
Maelezo ya picha, PSG inajipanga kumbakiza Neymar klabuni hapo mpaka 2025

Paris St-Germain wanaandaa mkataba mpya mpaka mwaka 2025 kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazili Neymar. Neymar, 28 atapata kitita cha euro milioni 38 (pauni milioni 33) kwa mwaka. (Sport - in Spanish)

Arsenal na Manchester United wanafikiria kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele,22. (Sport - in Spanish)

Inter Milan wako tayari kuweka kitita mezani cha pauni milioni 25 kwa ajili ya mshambuliaji wa Everton Moise Kean,20. (Express)

Kai Havertz
Maelezo ya picha, Man United wanataka kumsajili kiungo kinda wa Ujerumani Kai Harvertz

Manchester United wamemuongeza kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz,20, kwenye orodha yao ya wachezaji watakaotaka kuwasajili. (Standard)

Arsenal wanaweza kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 28 kwenda Atletico Madrid kama sehemu ya makubaliano ili kumpata kiungo wa kati wa Ghana Thomas Party ,26. (Sun)

Newcastle watatumia pauni milioni 200 kwa ajili ya wachezaji wapya na maendeleo ikiwa mapendekezo yao yatafanikiwa. (Mirror)

Rodrigo Moreno
Maelezo ya picha, Arsenal wamuulizia rasmi Moreno

Arsenal wameulizia rasmi uwezekano wa kumsajili winga wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 29. (Mirror)

Chelsea wanaandaa uhamisho wa mshambuliaji wa kikosi cha Freiburg Luca Waldschmidt wa gharama ya pauni milioni 20. (Sun)

Olivier Giroud
Maelezo ya picha, Olivier Giroud

Mshambuliaji wa Chelsea, Mfaransa Olivier Giroud,33, amefikia makubaliano binafsi na Inter Milan. (Tuttosport via Mail)

Mlinda mlango wa Burnley Joe Hart, 33, ananyemelewa na Derby na Besiktas. (Sun)

Kiungo wa zamani wa Manchester City na Arsenal Samir Nasri, 32,anatarajiwa kufukuzwa na Anderlecht kwa kushindwa kuwasiliana na Klabu wakati wa amri ya kutotoka nje kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (Derniere Huere via Mail)