The Cranes kuinyatia Taifa Stars CHAN

Timu ya The Cranes kutoka Uganda.
Maelezo ya picha, Timu ya The Cranes kutoka Uganda.
Iliyochapishwa

Timu ya taifa ya soka ya Uganda (The Cranes) itatumia mwaliko wa michuano ya kumbukumbu ya kimbali nchini Rwanda kujiandaa na mechi yake ya Michuano ya ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Tanzania

Taifa Stars imepangwa na Uganda kundi moja katika michuano ya CHAN ambazo fainali zake zitafanyika nchini Rwanda mwakani.

Stars itacheza na Uganda kati ya Juni 19, 20 na 21na mechi ya marudiano itachezwa kati ya Julai 3,4 na 5.

Kocha wa Uganda, Milutin Sredojevic “Micho” amekaririwa na vyanzo vya habari nchini Uganda akisema kuwa michuano hiyo ya Rwanda, itakayofanyika Juni 6-7 kuwakumbuka wana michezo waliokufa katika mauaji hayo ya mwaka 1994 itaipa Uganda mazoezi ya kutosha kuikabili Stars.

wachezaji wa The Cranes wakifurahia jambo
Maelezo ya picha, wachezaji wa The Cranes wakifurahia jambo

Kuelekea mechi hiyo ya timu hizo za Afrika ya Mashariki, tayari Micho alikaririwa katika siku za nyuma akisema kuwa anahitaji kutengeneza timu nzuri kuikabili Tanzania kwa sababu ina wachezaji waliokaa pamoja kwa muda mrefu na wengi wao wanacheza ligi ya nyumbani.

Kwa upande wa Stars, michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini Mei 18 itakuwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano hiyo ya CHAN dhidi ya Uganda, kwa mujibu wa kocha wa Stars, Mart Nooij.

.