Euro2016: 'Wahuni wa Urusi' warudishwa makwao

Iliyochapishwa
Makundi ya mashabiki wa Urusi yameanza kurudishwa nyumbani kufuatia msururu wa visa vya ghasia katika michuano ya Euro2016 nchini Ufaransa.
Polisi wa Ufaransa wemewalaumu wahuni 150 'waliofanyiwa mafunzo' kwa ghasia hizo kabla ya mechi kati ya Uingereza na Urusi iliochezwa mjini Marseille.

Chanzo cha picha, Reuters
Mashabiki sita wa Uingereza siku a Jumatatu walifungwa kutokana na majukumu yao katika ghasia hizo na UEFA imeonya kuzipiga marufuku timu zote mbili iwapo kutakuwa na ghasia zaidi.



























