Mazembe kucheza na Internacional

Iliyochapishwa

Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya dunia ya soka kwa upande wa vilabu, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumanne wanaingia uwanjani kupambana na Internacional ya Brazil.

Itakuwa ni nusu-fainali, na mashindano hayo yanafanyika Abu Dhabi.

TP Mazembe ilifanikiwa kuingia nusu-fainali, baada ya kuishinda Pachuca ya Mexico bao 1-0, katika pambano la robo-fainali.

Mbeza Bedi
Maelezo ya picha, Alifunga bao la pekee katika mechi dhidi ya Pachuca ya Mexico

Mbeza Bedi ndiye aliyepata bao hilo la pekee katika mechi hiyo, katika dakika ya 21, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Mulota Kabangu.

Mazembe, ambao wameweza kuhifadhi ubingwa wao barani Afrika, pia waliliwakilisha bara mwaka uliopita, lakini mchezo wao haukuvuma mbele ya vilabu vingine kutoka kote duniani.

Walishindwa mwaka jana katika mechi yao ya kwanza.

Kwa hiyo ni ufanisi mkubwa timu sasa imeweza kufika nusu-fainali.

Hii ni mara ya tatu, katika juhudi mara saba, kwa timu ya Afrika kuwa miongoni mwa timu nne zilizosalia katika mashindano ya vilabu kuwania Kombe la Dunia.

Timu ya Al Ahly ya Misri ilikuwa ya kwanza kufikia hatua hiyo mwaka 2006, na Etoile du Sahel ya Tunisia ilifikia kiwango hicho mwaka 2007.

This is only the third time in seven attempts that an African team has made the last four of the Club World Cup, after Al Ahly of Egypt in 2006 and Etoile du Sahel of Tunisia in 2007.