Heshima za mwisho kwa Nyangweso

Rais wa zamani wa chama cha Olimpiki nchini Uganda, Meja Jenerali Francis Nyangweso, alizikwa siku ya Jumamosi, 26 Februari 2011, nyumbani kwake Sofia, Busia, mpakani kati ya Uganda na Kenya.
Alizikwa kwa heshima zote za kijeshi, zilizoendeshwa na wanajeshi wa Uganda wa UPDF.

Mkurugenzi wa kamati ya ushirikiano wa kimataifa ya Olimpiki, Thomas Sithore, na mwanachama wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC), na vile vile rais wa Olimpiki, Kenya, Kipchoge Keino, ni kati ya wale waliowakilisha kamati hiyo ya michezo.
Sithore aliisoma risala ya rambirambi kutoka kwa rais wa IOC, Jacques Rogge.
Marehemu Nyangweso alifariki Jumanne, 22 Februari, baada ya kuugua.
Aliwahi kuwa kamanda katika jeshi la Uganda nyakati za rais Idi Amin, na aliviongoza vikosi vya nchi hiyo katika vita dhidi ya Congo mwaka 1962, na akipata nafasi pia kuwa waziri wa ulinzi.



























